Thursday, May 26, 2011

UTENGENEZAJI WA DVD YA KISWAHILI......

Kikundi cha ZINDUKA SOKA wakiwa kwenye mchezo wa kupitisha mpira kwenye chupa mara baada ya mapumzika ya zoezi la kutengeneza DVD kama kitendea kazi cha kocha wa zinduka soka anapokuwa mafunzoni ambayo yanawalenga hasa watoto chini ya miaka kumi hadi 14 katika mikoa mitatu Dar es Salaam, Morogoro na Iringa kwa lengo la kuelimisha jamii kuhusu Ukimwi na VVU unayofanyika Dar es Salaam kuanzia juzi. 
WAKIELEKEZWA






Tuesday, May 24, 2011

KESI YA EPA HIYO........



Rajabu Maranda na nduguye Farijala Hussein, wakipanda kwenye gari la polisi tayari kupelekwa Ukonga jana kwa ajili ya kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano jera baada ya kutiwa hatiani kwenye kesi yao iliyokuwa ikisikilizwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu Dar es Salaam

NDANI YA ULINZI MKALI ....




Hawaamini kama wanaenda jera.

Saturday, May 21, 2011

SAFARI YA Sheikh Yahya Hussein.






Ni vilio tu kila unayemuona amejawa na simazi za kuondokewa na mtabiri wetu wa nyote.











Waombolezaji wakiwa na jeneza la Sheikh Yahya Hussein kwenye maandamano ya kwenda kumzika, kutoka nyumbani kwake Magomeni Mwembechai hadi Msikiti wa Manyema kwa ajili ya kuswaliwa na hatimaye kwenye maziko yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza, yaliyopo Muhimbili, Dar es Salaam jana.

Rais Jakaya Kikwete, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, wakifuatilia maziko ya Sheikh Yahya Hussein, yaliyokuwa yakifanyika katika makaburi ya Tambaza, Dar es Salaam jana.
 
 Hapa ndio hatutamuona tena.

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

FURAHI LEO NA TABASAMU


Kwenye gari la abiria la kwenda mkoani si unajua kwamba kuna (temino) mapumziko kila baada ya safari, basi gari lilipofika, abiria kama kawaida yao wakashuka wakaenda kula na kupata mahitaji yao kama uchimba dawa na mengineyo, basi mmoja kati ya abiria alipanda na mayai matatu, na mhindi wa kuchemsha, abiria wenzake wakaaza kuguna mmmmmm! Alipogeuka wote wakanyamaza kwa kuwa jamaa alikuwa kajazia ile mbaya. Wakaendelea na safari mara jamaa akajamba, abiria wote tunakufa kwa harufu mbaya. Cheka kidogo usije jisahau…….. kama unakichekesho chochote tuma kwenye: JanethShekunde@yahoo.com nami nitakirusha kwa raha zako.

MAMBO YA HAPA NA PALE MTAANI.

 Fundi umeme kutoka katika shirika la umeme TANESCO akiwa juu akirekebisha mambo ya mwanga ili yawe sawa kama kawa katika jiji la Dar es Salaam.
Mpitanjia akishangaa miti iliyokatwa katika  eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, miti hiyo ilioteshwa kwa gharama kubwa hivi sasa inadaiwa eneo hilo linatakiwa kuwa kituo cha mabasi yaendayo mwendo kasi.
Shimo kama hili ni hatari likiwa barabarani kwa sababu linaweza kusababisha maafa za hapa na pale.
 KIJANA ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiokota chupa za plastiki za maji kwa ajili ya kuziuza viwandani pamoja na kwa akina mama wauzaji wa vinywaji (juisi). Eneo hilo la mto Kilungule analookota chupa hizo unadaiwa kutirishwa majitaka kutoka kwenye chemba za hostel za Mabibo jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wakazi wa Dar es Salaam.
Mwendesha pikipiki akiwa na jenereta akikatiza katika mitaa ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana, wakati akitoka kununua kwa ajili ya matumizi kutokana na mgawo wa umeme unaoendelea jijini. 
 Muuza mkaa akipitisha biashara yake hiyo mtaa hadi mtaa katika sehemu nyingi Dar es Salaam.

 Licha ya serikali kupiga marufuku mifugo kuzurura mitaani hovyo mbuzi hao walikutwa wakiwa magomeni mapipa Dar es Salaam jana bila ya kuwa na mchungaji jambo ambalo ni ukiuka wa sheria.

 


Muuza samaki katika soko la Feri jijini Dar es Salaam, akipanga samaki kwa ajili ya kuwauzia wanunuzi watakaofika katika soko hilo. Hivi sasa samaki wanapatikana kwa wingi katika soko hilo. Samaki mmoja aliuzwa kati ya Sh 10,000 na 15,000 badala ya Sh 20,000 hadi 25,000 kipindi cha nyuma.

 Askari polisi anayedaiwa kuwa msumbufu kwa waendesha pikipiki katika barabara ya BibiTiti Mohamed jijini Dar es Salaam,, akiwa amemkamata mwendesha pikipiki jana. Inadaiwa huwadai fedha kwa kila anayemkamata.
Mkazi jijini Dar es Salaam akimsaidia kumtwisha Mihogo Mama mfanyabiashara wa Mihogo eneo la Soko la Samaki Kivukoni, Dar es Salaam hivi karibuni.
 Muuzaji wa mahindi akiandaa biashara yake kwa ajili ya kuuza.

Gari la Serikali likiwa limejazwa magunia ya mkaa hadi pomoni kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu Jumapili iliyopita katika eneo la Utaho, kilomita chache nje ya Manispaa ya Singida.
 
Muuza dawa za asili  akiweleza wapitanjia eneo la soko la Kariakoo Dar es Salaam, jinsi nyoka anavyoweza kurusha mate na kumgonga  mtu na jinsi ya kujikinga na dawa zake  ambazo zinaondoa  sumu  kwa urahisi. 


Mfanyabiashara wa matunda akiwahudumia wateja wake huku biashara yake ikiwa wazi bila kujali afya za walaji wake kama alivyokutwa jana katika Mtaa wa Kongo Dar es Salaam. 
Maji machafu yakitiririka katika Barabara ya Kisutu, Dar es Salaam na kusababisha eneo hilo la barabara kuota mahindi kutokana na maji hayo yanayotiririka bila kufanyiwa marekebisho ya chemba iliyopasuka kwa kipindi kirefu sasa. 
 Chemba kama hizi hazitakiwe ni uchafu na uharibifu wa mazingira kwa hewa chafu hapa ni eneo la barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara wa samaki akielewana bei na mteja wake katika eneo la soko la feri jijini Dar es Salaam.