Monday, September 19, 2011

MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJILI


 Katibu wa WAYODE akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wenzake mjini Dodoma hivi karibuni


Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndula Products, Janet Mlowe, akimuonyesha moja ya mvinyo anaotengeneza Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Roberto Quiroz, wakati wa maonyesho ya wajasiriamali ambayo yameendeshwa na taasisi ya TWENDE, yaliyofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana.


Meneja Masoko wa Kampuni ya Mildor Group, Magdalena Chagile (Kulia) akiwauzia wateja waliotembelea kwenye maonyesho ya wiki ya wajasiriamali yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja hivi karibuni yaliyoandaliwa na TWENDE.

Waziri wa Maendeleo, Jinsia na Watoto, Sophia Simba akiangalia ubuyu bidhaa inayotengenezwa na Kampuni ya Mildor kwenye maonyesho ya wiki ya wajasiriamali yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja hivi karibuni yaliyoandaliwa na TWENDE. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Magdalena Chagile.

 WASHIRIKI WA MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI
Mkurugenzi Mkufunzi wa Kampuni ya Dimod Intergrated Awereness Solutions,Mahmoud Omary, akitoa mafunzo kwa wajasiriamali wakati wa semina ya mafunzo inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwenye Chuo cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.

Saturday, September 3, 2011

KUBORESHA

Mfanyabiashara wa vitu vya kuwekea maua, Godlove Ajuaye akipaka rangi chungu kwa ajili ya kukiweka tayari kwa kuuza kwa bei ya Sh. 15,000 hadi 25,000 kutegemea na ukubwa wake eneo la Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.

Thursday, September 1, 2011

KIND HEART AFRIKA KWA MALEZI BORA YA MTOTO

SERIKALI imeahidi kukidumisha na kukiendeleza kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Kind Heart Africa.
Hayo yalisemwa mjini Dar es Salaam juzi na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la kituo hicho.
Silaa alikiri kuwa serikali imekuwa ikijitolea katika kuendeleza sekta ya elimu, afya na nyinginezo lakini katika suala la kuwajengea watoto walio katika mazingira magumu maeneo ya kuishi ni kama vile imelitelekeza.
“Kutokana na umuhimu wa kuwathamini na kuhakikisha watoto walio katika mazingira magumu wanaishi salama na kupata huduma muhimu, wakati umefika kwa serikali kuwa mstari wa mbele kuwajengea vituo na kuvidumisha vile vilivyopo,” Meya Slaa alisema.
“Hivyo nitajitahidi pamoja na viongozi wengine waliopo chini yangu kuhakikisha tunakiendeleza kituo hiki, kwa kuwa wanaoishi hapa si wageni bali watoto wetu wa Kitanzania,” alisema.
Aidha aliutaka uongozi wa kituo hicho kuangalia namna itakavyopata wadau wengine watakaoshirikiana nao katika kumalizia baadhi ya maeneo ya kituo hicho.
Jengo lililogharimu sh. milioni 80 lilijengwa kwa udhamini wa raia wa India, Joshi Sathyavan.
Slaa pia alimpongeza Rais na Mchungaji wa madhehebu ya Buddha, Ilukpitiye Pannasekara, ambaye ni raia wa Sri Lanka kwa moyo wa huruma na upendo uliomfanya aje na wazo la kujenga kituo hicho kitakachowasaidia watoto wengi.
“Ni wajibu wa kila mmoja kutoa msaada wowote ukiwamo wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hiki ikiwamo kujenga uzio na majengo mengine ili kitimize malengo yake kwa watoto wetu,” aliongeza.
Naye Mchungaji wa Buddha Pannasekera aliishukuru serikali pamoja na wadhamini mbalimbali waliojitokeza kukamilisha ndoto yake ya kujenga kituo hicho cha kusaidia watoto walio katika mazingira magumu.
Hata hivyo, Mchungaji huyo alitoa wito kwa wadhamini wengine wenye moyo kujitokeza kwa wingi kukiendeleza kituo hicho ambacho kwa sasa kina watoto 27, wakiwemo wasichana watatu na wavulana 24.

UZINDUZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU ULIVYOKUWA KITUONI HAPO KIND HEART AFRIKA