Saturday, June 25, 2011

JAMII YETU

YAHEEE NTAFIKA TU……..
Mtu huyo akitumia nguvu nyingi kuvuta mkokoteni uliosheheni mizigo mkubwa kama alivyokutwa katika eneo la Malindi mjini Zanzibar juzi. Haikufamika mara moja alikuwa anaelekea wapi. Picha na Kulwa Karedia
Usafiri wa Zanzibar huo..... watu ni kuangaliana tu...
Askari wa Usalama akipima ili ajue kosa lipo kwa nani katika ajali, hakuna majeruhi wote wazima.
 HATARI SANA
 KAZI HIYO..
 BURUDANI


Mchezaji wa tenesi, Abigail Mburu, akipiga mpira wakati wa mafunzo ya mchezo huo yanayofanyika katika uwanja wa kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.

Friday, June 17, 2011

JAMII YETU.

NANI ATATUOKOA?
Kutokana na uhaba wa nishati ya gesi kukosekana katika maeneo mbalimbali hasa vijijini, wananchi wamelazimika kutumia kuni kwa ajili ya mahitaji ya nyumbani, kama mwanamke huyo alivyokutwa juzi Wilayani Kilombero, mkoani Morogoro akiwa amejitwisha mzigo wa kuni.
 HAPA AKIWA AMELALA KWA AJILI YA NJAA KALI.
Mtoto, Daudi Lafa Chengula, aliyetokea Mkoa wa Iringa kuja Dar es Salaam bila kuwa na ndugu yeyote wa kumsaidia, kwa sababu ya maisha magumu vijijini akihojiwa na wasamalia wema katika eneo la hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam jana.
 
SIO HAKI.
Watoto, wakiwa wamebeba chupa za maji walizookota Ubungo jijini Dar es Salaam jana, katika kituo cha mabasi yaendayo mkoani kwa ajili ya kuuza na kupata pesa za mahitaji.
Mwendesha baiskeli yenye matairi matatu (guta), akiwa amebeba abiria aliyekaa bila kuhofia usalama wa maisha yake katika eneo la Keko, Dar es Salaam.

Mwendesha pikipiki akiendesha pikipiki yake iliyosheheni mikate na kushindwa kuona nyuma jambo linalohatarisha maisha yake kwani anaweza kugongwa na gari linalotoka nyuma yake.

Saturday, June 11, 2011

MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI TGNP

MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba nchini Deus Kibamba ameitaka jamii iwe na uvumilivu katika kipindi hiki cha mchakato wa kuandaa katiba mpya.
 Hatua hiyo imefikia baada ya kuonekana mitazamo mipya ya wadau  ambayo inalenga ukusanyaji wa maoni ya sehemu mbalimbali na kuifanya katiba mpya iwe ya kudumu.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya uandishi wa katiba mpya jijini Dar es Salaam jana, Kibamba alisema, katiba lazima ilenge mawazo ya watu wote bila kuwasahau wananchi walioko vijijini ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha.
Aliendelea kusema “hatuna katiba iliyoandaliwa kwa kushirikisha watu wote kwa kutoa fursa sawa zisizo lenga manufaa ya watu fulani, tunataka tuandae katiba itakayolenga maoni ya watu  wa Taifa zima na sio wachache, kuandaa katiba hakuitaji mawazo ya wanataaluma peke yao kama wengi wanavyo dhani , mchakato huu utamlenga kila mmoja inambidi kuandaa katiba ambayo haibagui na kuangalia jinsia.”
Kibamba anahimiza Serikali kutoa fursa sawa za uongozi kwa nafasi za juu kwa wanawake badala ya  kupewa nafasi za upendeleo kwa kuwa nayo wanamchango mkubwa katika kutoa mawazo.

WAANDISHI WALIPOKUWA KWENYE MAFUNZO.

 Mtoa mada kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyonalengo la kuandaa kuandika katiba mpya na tamasha la mwaka linalotarajiwa kufanyika september mwaka huu.
 Naye msimamizi katika kitengo cha uenezi wa habari TGNP, Dada Kemy, akitoa maelekezo kwa waandishi hawo.

 Vile vile Ofisa Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Deo Temba, akitoa mawazo katika mafunzo hayo.
 Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mjini na mikoani wakisikiliza kwa makini

 Mchoraji wa katuni kutoka kampuni ya The guardian, Muhidin Msamba, akichangia jambo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo.
 Mtoa mada kutoka mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Eluka Kibona, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu tamasha linalitarajiwa kufanyika chini ya uongozi wa mtandao huo.
 Mwandishi Mwanaharakati kutoka Gazeti la Dira ya Mtanzania, Pendo Omary Juma, akiwaelekeza waandishi wenzake wakati wa kuchangia mada.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa kufunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa kufunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo jana.
HAPO ILIKUWA MWISHO Naibu Mkurugenzi aliwashukuru sana waandishi wa habari kwa kujitoa kwa moyo kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuandika habari za kijamii hasa kuwalenga zaidi wale walio pembezoni mwa nchi yetu kwa kuwa ndio wanapata shida sana katika kujitoa kwenye maisha, na muda mwingi wao hutumia kwa kutafuta kuni, chakula, maji, na mahitaji mengine.

Thursday, June 9, 2011

MAMBO YA JAMII

 Wauza maji wakisaka wateja katika kituo cha mabasi cha Temeke jijini Dar es Salaam, chupa moja ya maji inauzwa kati ya Sh 300 hadi 500.
 Mgambo wa Manispaa ya jiji wakiwa kwenye kazi, kuhakikisha kila mfanyabiashara anafanya biashara katika eneo husika.
 Muuza karanga akisaka wateja katika eneo la Temeke jijini Dar es Salaam, fungu la karanga huuza Sh 500.

 Mfanyabiashara wa Majeneza katika eneo la Manzese.
 Mtoto ambaye alitakiwa awe darasani kutokana na kipato kuwa kidogo hulazimika kuokota chupa za maji kwa ajili ya kuuza ili kuongeza kipato katika familia.
Hii ni hatari kwa mtoto kukaa nyuma bila kizuizi chochote,kuhatarisha maisha.

Wednesday, June 1, 2011

MAMBO YA MTAANI NA JAMII YETU

Mgambo wa Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, wakiwa kwenye ulinzi mkali wa raia wanaopendelea kupumzika na kufanyia biashara zao katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi, bila kujali sehemu hiyo imewekwa kwa ajili ya kupendezesha jiji.
 
Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, wakiwa katika makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi, jijini Dar es Salaam, wakigawana juisi kwenye chupa kutokana na njaa inayowapata watoto hao wanapotafuta chakula wenyewe bila ya msaada wowote, sehemu ya kulala na mavazi
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Manzese, Dar es Salaam, wakichimba shimo la taka baada ya kupewa adhabu na mwalimu wao, walipokutwa wakipiga kelele darasani wakiwa wamekaa chini.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Juma Nkamia, akiwa na wajumbe wenzake wa kamati hiyo wakiwangalia kwa huzuni wafanyakazi wa Kinwanda cha Jambo Plastics kilichopo barabara ya Nyerere Dar es Salaam, wakiwa na mavazi yao rasmi ya kazi kaptura na Tshets kwa wanaume na wanawake, wabunge hao nusura walie kutokana na wafanyakazi hao kufanywa kama watumwa katika nchi yao.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kata Manzese, Dar es Salaam, wakichimba shimo la taka baada ya kupewa adhabu na mwalimu wao, walipokutwa wakipiga kelele darasani wakiwa wamekaa chini.
 
Uzio ukiendelea kuanguka katika eneo la Manzese Darajani, Dar es Salaam, baada ya uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kutokuwa na mbinu mbadala za kuujenga upya.

 














 Balozi wa kampeni ya OTESHA, Steven Kanumba, akikata utepe.





Mkurugenzi wa OXFAM akiweka saini.