Friday, February 24, 2012

MICHEZO MBALIMBALI NA MATUKIO YA MTAANI

 
Nahodha wa timu ya mpira wa mguu kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Good Samaritan, Abdillah Barakat, akikabidhiwa kombe na mgeni rasmi, Sakina Shiraz, (katikati) mara baada ya ushindi kwenye uwanja wa michezo Chuo Kikuu Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mratibu wa Shule hiyo, Jarzana Mussaji na Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Arseniks Ndege.
 Mchezaji wa timu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Good Samaritan, Khaleed Nurdin, akipiga mpira wakati wa mechi dhidi ya kidato cha tatu uliyofanyika katika uwanja wa chuo kikuu Dar es Salaam jana.

 Mchezaji wa mpira wa mkono Kidato cha Nne, Suhail Alibhai, akipiga mpira wakati wa mechi dhidi ya kidato cha pili wote ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Good Samaritan kwenye uwanja wa Chuo kikuu  Dar es Salaam  jana.

 Mtoto akiokota chupa kwa ajili ya kujipatia kipato
Hali ngumu ya maisha inamlazimu kufanya kazi kama hii ili kuongeza kipato

Friday, February 17, 2012

YALIYOJIRI MITAANI WIKI HIIII

 Mfanyabiashara katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam akijipatia kipato kwa kuuza machungwa, kwa bei ya sh. 200 hadi 250 kwa moja.
 HAYA SASA KIZAA ZAA Kigamboni
 Mambo ya  SUN RISE beach  Mjimwema jamani, ukienda unatakiwa kuwa na vitu kama hivi kwa ajili ya kuogelea
 Kivuko hichi hivi sasa tangu nauli ipande hakuna hata upungufu wa abiria zaidi yake wamezidi kuongezeka kutoka sehemu mbalimbali kutembelea vivutio vya Kigamboni.
Biashara nyingine jamani zinastabisha watu, Mfanyabiashara huyu akipiti pembeni mwa barabara ya Kigamboni kutembeza madumu na ndoo kwenye maduka.
 Mambo ya usafiri wa bodaboda katika barabara ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakisubiri abiria kuwapeleka sehemu mbalimbali.
Mdau wa blog hii, Elias Mkapa akiwa amepozi nje ya ukumbi wa Sunrise jijini Dar es Salaam



HAYA SASA UKIONA, KOBE KAINAMA UJUE ANATUNGA SHERIA!!
WENGINE WATAJIULIZA SHERIA GANI HIYOOO???? UTAJIONEA WIKI IJAYO.