Wednesday, August 24, 2011

Hafla fupi ya kuwaapisha Walimu waliojitolea kuwasaidia Watanzania kwa kutumia Elimu yao katika Mikoa mbalimbali Nchini ilivyokuwa kwenye Ukumbi wa Nyumbani kwa Balozi wa Marekani Masaki jijini Dar es Salaam jana.


 KUIGIZA SASA
 WATU WALIPENDEZA KAMA KAWAIDA
 BURUDANI MBALIMBALI WEE ACHA TU




 WAKATI  NDIO HUO



Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt (katikati), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba na Andrea Wajnar-Diagnne wa Peace Coaps Tanzania Country Director,  wakila keki baada ya kumalizika hafla ya kuapishwa walimu wa kujitolea kutoka marekani ambao watafanya kazi nchini kwa miaka 2 .


Friday, August 19, 2011

WAMAMA WANAVYOWAJIBIKA KWENYE KAZI YA USAFI WA JIJI


 Hapa wakifanya usafi katika barabara ya shekilango jijini Dar es Salaam, wamama hawa wanapenda kazi yao sana lakini tatizo kubwa linaliwapata ni ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi hiyo ngumu ambayo inahitaji kila siku unaporudi nyumbani upate lita moja la maziwa. Wafanyausafi hawa wanalalamika mishahara kuwa midogo sana.

 Vitu vya kutengenezea sabuni ya maji
 Mwalimu akisisitiza jambo kwa wajasiliamali wakati akitoa somo

 SABUNI NDIO HIYO TAYARI

Tuesday, August 16, 2011

Siku ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika viwanja vya Mnazi moja jana jinsi yalivyokuwa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo ya ubora wa thamani za ndani kutoka kwa Mkurugenzi wa Jaffer Ind.Sain Ltd ,Vishal Sing Sain  zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa kutumia Malighafi inayopatikana nchini Tanzania wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana.



Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa, Elizabeth Munuo, ambayo yalielezea jinsi kinyago alichoshika kilivyokuwa kinatumika katika sherehe za ngoma binti anapokuwa hapo zamani, katika uzinduzi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika  mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali na wananchi wakiangalia mfano wa nyumba katika uzinduzi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika,uliotengenezwa na wanafunzi wawili, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kitado cha pili wote wa shule ya Sekondari ya Tandika Wilaya ya Temeke Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja jana.




 MAANDAMANO NDIO HAYO



 ZAWADI BABU KUBWA
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo ngoma Hamisi Mnyupe(kushoto),Roman Mng’ande(katikati) na Eddo Sanga(kulia) wakiwajibika jukwaani katika uzinduzi wa  maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika  mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana katika viwanja vya Mnazi moja jana.


 MAMBO YA ZAWADI SASA
Muuza Tende, Sophia Hamisi, akiuza tende nje ya Soko la Kariakoo jana. Tende huuzwa kwa Sh. 300 hadi 1000.
 MAMBO YA BIASHARA HAYO
Mfanyabiashara wa mayai akiweka bidhaa sawa kwa ajili ya kuuza kwa wateja wake katika soko la Kisutu jiji Dar es Salaam

Friday, August 12, 2011

WATOTO WANAVYOPATA TABU YA MAISHA

Wakati juzi ilikuwa siku ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti na mpango wa kitaifa wa kushughulikia ukatili kwa watoto na mpango wa udhibiti wa taifa, mpango huo hautafanikiwa ikiwa juhudi kubwa hazitaelekezwa kusaidia watoto kama hawa wanaoishi katika mazingira magumu, kama wanavyoonekana pembeni ya Barabara ya Samora, jijini Dar es Salaam juzi.

 Uzinduzi wa Chama cha Umoja wa Wanafunzi waliosomea  nchini China ulivyokuwa Dar es Salaam

PICHA YA PAMOJA NA BALOZI wa China nchini, Liu Kinsheng wa (tatu kulia).

Saturday, August 6, 2011

SIKU YA MAOMBEZI KWA WAPENDWA WETU WA NORWAY.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Kihindu Tanzania, Dinesh Vaishnau, akiwa na baadhi ya washiriki walioshiriki kwenye kumbukumbu ya vifo vya raia wa Norway, ambao walipoteza maisha kwa mlipuko wa  mabomu hivi karibuni. Ibada hiyo ilifanyika katika ofisi za ubalozi wa nchi hiyo  Dar es Salaam jana.


 WALIOHUDHURIA NI WATU KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI








 TUNAWAKUMBUKA KWA SALA
Mchungaji wa dhehebu la Bhudha kutoka nchi ya Sri Lanka nchini, Ilukpitiye Pannasekara, akisali kwenye ibada ya kumbukumbu ya vifo vya raia wa Norway ambao walipoteza maisha kwa mlipuko wa bomu ijumaa iliyopita nchini Norway. Ibada hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Balozi wa Norway nchini, Svein Baera.