Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo ya ubora wa thamani za ndani kutoka kwa Mkurugenzi wa Jaffer Ind.Sain Ltd ,Vishal Sing Sain zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwa kutumia Malighafi inayopatikana nchini Tanzania wakati wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meshak Sadick akisikiliza maelekezo kutoka kwa Katibu Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa, Elizabeth Munuo, ambayo yalielezea jinsi kinyago alichoshika kilivyokuwa kinatumika katika sherehe za ngoma binti anapokuwa hapo zamani, katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana.
Wanafunzi wa Shule mbalimbali na wananchi wakiangalia mfano wa nyumba katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika,uliotengenezwa na wanafunzi wawili, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kitado cha pili wote wa shule ya Sekondari ya Tandika Wilaya ya Temeke Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa Mnazi Mmoja jana.
MAANDAMANO NDIO HAYO
ZAWADI BABU KUBWA
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo ngoma Hamisi Mnyupe(kushoto),Roman Mng’ande(katikati) na Eddo Sanga(kulia) wakiwajibika jukwaani katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jana katika viwanja vya Mnazi moja jana.
MAMBO YA ZAWADI SASA
Muuza Tende, Sophia Hamisi, akiuza tende nje ya Soko la Kariakoo jana. Tende huuzwa kwa Sh. 300 hadi 1000.
MAMBO YA BIASHARA HAYO
Mfanyabiashara wa mayai akiweka bidhaa sawa kwa ajili ya kuuza kwa wateja wake katika soko la Kisutu jiji Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment