MWENYEKITI wa Jukwaa la Katiba nchini Deus Kibamba ameitaka jamii iwe na uvumilivu katika kipindi hiki cha mchakato wa kuandaa katiba mpya.
Hatua hiyo imefikia baada ya kuonekana mitazamo mipya ya wadau ambayo inalenga ukusanyaji wa maoni ya sehemu mbalimbali na kuifanya katiba mpya iwe ya kudumu.
Akizungumza wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya uandishi wa katiba mpya jijini Dar es Salaam jana, Kibamba alisema, katiba lazima ilenge mawazo ya watu wote bila kuwasahau wananchi walioko vijijini ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha.
Aliendelea kusema “hatuna katiba iliyoandaliwa kwa kushirikisha watu wote kwa kutoa fursa sawa zisizo lenga manufaa ya watu fulani, tunataka tuandae katiba itakayolenga maoni ya watu wa Taifa zima na sio wachache, kuandaa katiba hakuitaji mawazo ya wanataaluma peke yao kama wengi wanavyo dhani , mchakato huu utamlenga kila mmoja inambidi kuandaa katiba ambayo haibagui na kuangalia jinsia.”
Kibamba anahimiza Serikali kutoa fursa sawa za uongozi kwa nafasi za juu kwa wanawake badala ya kupewa nafasi za upendeleo kwa kuwa nayo wanamchango mkubwa katika kutoa mawazo.
WAANDISHI WALIPOKUWA KWENYE MAFUNZO.
Mtoa mada kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyonalengo la kuandaa kuandika katiba mpya na tamasha la mwaka linalotarajiwa kufanyika september mwaka huu.
Naye msimamizi katika kitengo cha uenezi wa habari TGNP, Dada Kemy, akitoa maelekezo kwa waandishi hawo.
Vile vile Ofisa Habari wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Deo Temba, akitoa mawazo katika mafunzo hayo.
Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mjini na mikoani wakisikiliza kwa makini
Mchoraji wa katuni kutoka kampuni ya The guardian, Muhidin Msamba, akichangia jambo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo.
Mtoa mada kutoka mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Eluka Kibona, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu tamasha linalitarajiwa kufanyika chini ya uongozi wa mtandao huo.
Mwandishi Mwanaharakati kutoka Gazeti la Dira ya Mtanzania, Pendo Omary Juma, akiwaelekeza waandishi wenzake wakati wa kuchangia mada.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa kufunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo jana.
Kaimu Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati wa kufunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyokuwa yanatolewa na taasisi hiyo jana.
HAPO ILIKUWA MWISHO Naibu Mkurugenzi aliwashukuru sana waandishi wa habari kwa kujitoa kwa moyo kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuandika habari za kijamii hasa kuwalenga zaidi wale walio pembezoni mwa nchi yetu kwa kuwa ndio wanapata shida sana katika kujitoa kwenye maisha, na muda mwingi wao hutumia kwa kutafuta kuni, chakula, maji, na mahitaji mengine.
No comments:
Post a Comment