Fundi umeme kutoka katika shirika la umeme TANESCO akiwa juu akirekebisha mambo ya mwanga ili yawe sawa kama kawa katika jiji la Dar es Salaam.
Mpitanjia akishangaa miti iliyokatwa katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam, miti hiyo ilioteshwa kwa gharama kubwa hivi sasa inadaiwa eneo hilo linatakiwa kuwa kituo cha mabasi yaendayo mwendo kasi.
Shimo kama hili ni hatari likiwa barabarani kwa sababu linaweza kusababisha maafa za hapa na pale. KIJANA ambaye jina lake halikufahamika mara moja, akiokota chupa za plastiki za maji kwa ajili ya kuziuza viwandani pamoja na kwa akina mama wauzaji wa vinywaji (juisi). Eneo hilo la mto Kilungule analookota chupa hizo unadaiwa kutirishwa majitaka kutoka kwenye chemba za hostel za Mabibo jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wakazi wa Dar es Salaam.
Mwendesha pikipiki akiwa na jenereta akikatiza katika mitaa ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam jana, wakati akitoka kununua kwa ajili ya matumizi kutokana na mgawo wa umeme unaoendelea jijini.
Muuza mkaa akipitisha biashara yake hiyo mtaa hadi mtaa katika sehemu nyingi Dar es Salaam.
Licha ya serikali kupiga marufuku mifugo kuzurura mitaani hovyo mbuzi hao walikutwa wakiwa magomeni mapipa Dar es Salaam jana bila ya kuwa na mchungaji jambo ambalo ni ukiuka wa sheria.
Muuza samaki katika soko la Feri jijini Dar es Salaam, akipanga samaki kwa ajili ya kuwauzia wanunuzi watakaofika katika soko hilo. Hivi sasa samaki wanapatikana kwa wingi katika soko hilo. Samaki mmoja aliuzwa kati ya Sh 10,000 na 15,000 badala ya Sh 20,000 hadi 25,000 kipindi cha nyuma.
Askari polisi anayedaiwa kuwa msumbufu kwa waendesha pikipiki katika barabara ya BibiTiti Mohamed jijini Dar es Salaam,, akiwa amemkamata mwendesha pikipiki jana. Inadaiwa huwadai fedha kwa kila anayemkamata.
Mkazi jijini Dar es Salaam akimsaidia kumtwisha Mihogo Mama mfanyabiashara wa Mihogo eneo la Soko la Samaki Kivukoni, Dar es Salaam hivi karibuni.
Muuzaji wa mahindi akiandaa biashara yake kwa ajili ya kuuza.
Gari la Serikali likiwa limejazwa magunia ya mkaa hadi pomoni kama lilivyokutwa na mpiga picha wetu Jumapili iliyopita katika eneo la Utaho, kilomita chache nje ya Manispaa ya Singida.
Muuza dawa za asili akiweleza wapitanjia eneo la soko la Kariakoo Dar es Salaam, jinsi nyoka anavyoweza kurusha mate na kumgonga mtu na jinsi ya kujikinga na dawa zake ambazo zinaondoa sumu kwa urahisi.
Mfanyabiashara wa matunda akiwahudumia wateja wake huku biashara yake ikiwa wazi bila kujali afya za walaji wake kama alivyokutwa jana katika Mtaa wa Kongo Dar es Salaam.
Maji machafu yakitiririka katika Barabara ya Kisutu, Dar es Salaam na kusababisha eneo hilo la barabara kuota mahindi kutokana na maji hayo yanayotiririka bila kufanyiwa marekebisho ya chemba iliyopasuka kwa kipindi kirefu sasa.
Chemba kama hizi hazitakiwe ni uchafu na uharibifu wa mazingira kwa hewa chafu hapa ni eneo la barabara ya Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara wa samaki akielewana bei na mteja wake katika eneo la soko la feri jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment