Saturday, May 14, 2011

MAMBO YA MISS DAR CITY CENTER


 Mwanzo mwisho burudani......

 Miss wanajiweka tayari kwa mashindano..

 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, naye alikuwapo (Kushoto) ......







 Tano bora wakijiweka sawa......

 Mazungumzo sasa...... Burudani chini....
 Msanii wa kizazi kipya, Tunda, naye yupo kazini.....

 Mshindi wa Shindano la Miss Dar City Center, Alexia William (katikati) akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wakati wa shindano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Lamada Dar es Salaam juzi.Kushoto ni mshindi pili, Salha Israel na  wa tatu Jeniffer Kakolaki. Picha za Chini




Warembo wakifurahi kwa raha zao baada ya kushinda.

Thursday, May 12, 2011

MAMBO MAZURI CRDB.......


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, DK. Charles Kimei, akitoa hotuba fupi kwa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na washiriki kutoka sehemu mbalimbali kabla ya kuweka saini mkataba wa hali bora za wafanyakazi kati ya Chama cha Wafanyakazi  wa Taasisi ya Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) na menejimenti ya benki ya hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Washiriki sasa ndio kama hawa katika kuhakiki kama ni kweli.

 Meza kubwa...

Wakisaini sasa mkataba huo, kushoto ni Katibu Mkuu wa TUICO Taifa, Jonathan Peleshi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. 

Wanabadilishana sasa mkataba baada ya kusaini. Kulia ni Ofisa Mawasiliano wa ILO, Magnus Minja

Zikafuatiwa na picha za pamoja kwa viongozi kutoka TUICO na CRDB.





Katibu Mkuu wa TUICO, Jonadhan Peleshi, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Benki hiyo, Dorah Ngauga.
 UBUNIFU WA MAVAZI SASA........
Mwenyekiti wa Asasi ya Tanzania Women Progressive Trust Fund, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu kazi zake za ubunifu wa mavazi na onyesho la mavazi yake ya kitamaduni yatakayofanyika kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kuanzia saa 2:00 usiku.
Mavazi yenyewe yatakuwa ya aina mbalimbali kulingana na nyakati shughuli hisika alisema Hilda Bandio, na nyote mnakaribishwa kesho bila kukosa.

Monday, May 9, 2011

YALIYOJIRI MITAANI

 Mfanyabiashara wa nyama akisubiri wateja kwa hamu buchani mwake.
 Mama akiuza samaki ili kuongeza kipato.
 Mfanyabiashara wa biashara ndogondogo akitembeza bidhaa zake katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Maji yakiwa yamefurika juu shimo katika eneo la chuo cha ustawi wa jamii jana jijini Dar es Salaam
Kila mtu na Biashara yake ili tu aing'ize kipato.

Thursday, May 5, 2011

ZAWADI NZURI.

 Balozi wa Misri, akikitoa maelezo ya zawadi kwa niaba ya serikali yao.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Saidi Mwema, akikabidhiwa zawadi na Balozi wa Misri nchini, Wael Adel Nasr.
 Balozi wa Misri nchini, Wael Adel Nasr, akizungumza jambo wakati wa sherehe hiyo.
 Waliyohudhuria sherehe hiyo ya makabidhiano
Kikundi cha Polisi wakiburudisha.

Monday, May 2, 2011

MGOMO WA MADEREVA, KILIO KWA ABIRIA

 Mambo ya maonyesho ya mavazi ya harusi.
 Abiria wakitafakari jinsi ya kuondoka.
 Kituo cha Kitaifa hakitakiwe kiwe kama hivi jamani.
 Abiria wakishangaa basi zilizokuwa zimepaki.
 Hawa nao wanadai warudishiwe nauli zao.....
 Mambo ndio kama haya jana hiyo........
 Hawa sijui hawana kazi. 
 Basi zinaaza safari sijui ni saa ngapi kufika.
 Washangiliaji sasa kama mechi.


Safari zipo muda wowote kutoka sasa mgomo kwa heri.