Wednesday, May 18, 2011

JAMII YETU NA MAMBO YAKE

 Viazi vitamu fungu sh. 1,000 hadi 500
 Zao la viazi likiwa sokoni kwa bei nafuu ndoo sh.10,000 hadi 15,000.
 Mtoto kama huyu anatakiwa kuwa shule wala sio kuwa kwenye biashara kama anavyoonekana akiwa na masikitiko ya jinsi gani ataweza kutoka kimaisha.
 Viazi ni bora kwa afya zetu.
Mfanyabiashara huyu akiwa kwenye mawazo ya biashara yake kuwa kama itafanikiwa kuisha kwa siku hiyo.

BURUDANI ZA ASILI NI MUHIMU...


Wanne na kundi lake wakiburudisha wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya Kampuni ya Vinywaji Pepsi (SBC).
 Burudani  raha tuu....
 Sarakasi kama kawa



 Moto huoooo...


 FM Academia nawo hawakurudi nyuma...chini





Miaka kumi hiyooo...

Saturday, May 14, 2011

Msama Promotions yatoa mil 4 kwa wajane



Na Mwandishi Wetu.
HATIMAYE Msama Promotions waandaaji wa Tamasha kubwa la Pasaka wamekamilisha ahadi yake ya kuwasaidi wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kwa kuwakabidhi wajane 24 fedha taslimu sh. 150,000 kila mmoja.
 Akikabidhi fedha hizo, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, alisema kwamba sasa ametimiza ahadi aliyoitoa wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka lililofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee huku mgeni rasmi akiwa ni rais wa jamhuri wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
 Aidha Msama alisema kwamba fedha hizo zimepatikana kutokana na mauzo ya albamu ya Haleluya Colletion Vol 5 ambayo ilizinduliwa katika Tamasha la Pasaka.
 “Leo tunatimiza ahadi yetu ya kuwapatia wanawake wajane fedha za mitaji ya biashara kama ambavyo tuliahidi wakati wa maandalizi ya tamasha la Pasaka,” alisema Msama
 Wanawake hao wajane waliokabidhiwa fedha hizo za mitaji wametoka katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo jumla ya shilingi milioni 4 zimetumika.
Pia fedha fedha zilizopatikana kwenye Tamasha hilo zitatumika kuwasaidia kuwasomesha watoto yatima.
Msama Promotions tayari imeshatoa msada wa shilingi milioni tatu kwa waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

MAMBO YA MISS DAR CITY CENTER


 Mwanzo mwisho burudani......

 Miss wanajiweka tayari kwa mashindano..

 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, naye alikuwapo (Kushoto) ......







 Tano bora wakijiweka sawa......

 Mazungumzo sasa...... Burudani chini....
 Msanii wa kizazi kipya, Tunda, naye yupo kazini.....

 Mshindi wa Shindano la Miss Dar City Center, Alexia William (katikati) akipunga mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wakati wa shindano hilo lililofanyika kwenye Hoteli ya Lamada Dar es Salaam juzi.Kushoto ni mshindi pili, Salha Israel na  wa tatu Jeniffer Kakolaki. Picha za Chini




Warembo wakifurahi kwa raha zao baada ya kushinda.

Thursday, May 12, 2011

MAMBO MAZURI CRDB.......


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, DK. Charles Kimei, akitoa hotuba fupi kwa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na washiriki kutoka sehemu mbalimbali kabla ya kuweka saini mkataba wa hali bora za wafanyakazi kati ya Chama cha Wafanyakazi  wa Taasisi ya Fedha, Viwanda, Biashara, Huduma na Ushauri (TUICO) na menejimenti ya benki ya hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana.

Washiriki sasa ndio kama hawa katika kuhakiki kama ni kweli.

 Meza kubwa...

Wakisaini sasa mkataba huo, kushoto ni Katibu Mkuu wa TUICO Taifa, Jonathan Peleshi na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. 

Wanabadilishana sasa mkataba baada ya kusaini. Kulia ni Ofisa Mawasiliano wa ILO, Magnus Minja

Zikafuatiwa na picha za pamoja kwa viongozi kutoka TUICO na CRDB.





Katibu Mkuu wa TUICO, Jonadhan Peleshi, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba huo. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Benki hiyo, Dorah Ngauga.
 UBUNIFU WA MAVAZI SASA........
Mwenyekiti wa Asasi ya Tanzania Women Progressive Trust Fund, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu kazi zake za ubunifu wa mavazi na onyesho la mavazi yake ya kitamaduni yatakayofanyika kesho katika ukumbi wa Ubungo Plaza kuanzia saa 2:00 usiku.
Mavazi yenyewe yatakuwa ya aina mbalimbali kulingana na nyakati shughuli hisika alisema Hilda Bandio, na nyote mnakaribishwa kesho bila kukosa.