Saturday, January 28, 2012

BIASHARA MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mitego ya panya sh. 1000 inaua kweli kweli pata wako
 TAMUUUU: ILE SANA

MIHOGO MIHOGO SH. 2000 MMOJA NA KIPANDE SH. 200

Saturday, January 21, 2012

 Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni umekataza kutokuwa na gereji bubu kama hii hapa, huu ni uchafuzi wa mazingira.


Madereva wa pikipiki aina ya TOYO wakisubiri abiria katika soko la Buguruni jijini Dar es Salaam
 NYANYA sasa ni adimu kwa kipindi hiki ndoo moja ndogo ni sh. 6,000 bila punguzo.
 MAZOEZI YA MICHEZO MBALIMBALI SASA


 Emilian Katabaro kazi sasa.

 MAMBO YA TASWA

Friday, January 13, 2012

MICHEZO MBALIMBALI YA SOKA NCHINI



Kipa wa timu ya Ngome ya Lugalo ya mpira wa magongo, Cosmas Bukoke, akizuia mpira wakati wa mashindano ya phoenix assurance mapinduzi yaliyoanza kuchezwa kwenye Uwanja wa mpira wa magongo Lugalo, Dar es Salaam jana. Timu ya magereza ilishinda bao 8-0.














Mmoja wa wachezaji wa Simba SC walio chini ya umri wa miaka 14 akiruka mazoezini kujiandaa na mechi ya kirafiki na timu ya kituo cha Chipukizi cha Sinza itakayochezwa mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam jana.

 KASEJA WA BAADAE
 KUMBUKUMBU
MARYSA  JACOB
NI MIAKA MIWILI SASA TANGU UTUTOKE TULIKUPENDA SANA ILA MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI, TUNAJUA KIMWILI HAUPO NASI ILA KIROHO  TUPO PAMOJA; TUNAKUKUMBUKA SANA TUKIKUMBUKA UCHESHI  WAKO, TABASAMU LAKO NA MENGI TULIOKUWA TUKIFANYA PAMOJA,  Mimi Mama yako Janeth Shekunde, Bibi yako, Rahel Shekunde, Dada zako, Careen, Rahel, Veronica, Dora na ndugu wengine wanakukumbuka sana.

MWANGA WA MUNGU UKUMURIKIE MILELE UPUMZIKE KWA AMANI AMINA. 
 Nitazidi kukukumbuka mwanangu mpenzi.

Saturday, January 7, 2012

ZIARA YA MKURUGENZI WA INUKA MJINI TANGA

 Wajasiriamali wakisikiliza mafunzo kwa makini
Mkurugenzi wa Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Inuka, David Msuya, akitoa mafunzo ya kuendeleza biashara kwa wajasiriamali wadogowadogo kwa vikundi 13  vilivyopo wilaya ya  Mkinga jijini Tanga.




 KANISANI SASA
 Kusifu na Kuabudu vilitawala Magomeni Calvary jijini Tanga

 TUNASIKILIZA KWA MAKINI MAHUBIRI
 MAOMBI SASA: UTAPONA KWA JINA LA YESU
 MNAELEWA JAMANI INJILI SIO LELE MAMA
 HAWA NAO WANAJIPATIA KIPATO KULIKO KUIBA
 MATUNDA SAFI HAYA

 Mama mjasiriamali anauliza swali kwa Mkurugenzi wa Inuka, David Msuya, baada ya kumaliza mafunzo
KAMA HUJAELEWA ULIZA SWALI usijeondoka hujaelewa kitu

VIKUNDI 13 vya wajasiriamali wadogodogo Wilayani Mkinga jijini Tanga wamefaidika na mpango maalumu wa elimu ya namna ya kuviendeleza vikundi vyao ikiwemo kukopa na kulipa ikiwa lengo ni kumuenua katika kukabiliana na ushindani wa ubora wa bidhaa kwenye masoko ya kimataifa.

Akizungumza katika warsha ya siku moja Wilayani hapa jana, Mwenyekiti wa Taasisi ya Inuka David Msuya, alisema lengo la Taasisi hiyo ni kuwaona Wajasiriamali  hasa wa kike wakifanya kazi zao kwa malengo ikiwa na pamoja na faida.

Alisema vikundi hivyo vitapatiwa mafunzo ya namna ya kuweza kuanzisha miradi ya kutengeneza Sabuni, Mishumaa, mabatiki,na bidhaa nyingine kwa awamu tofauti huku baadhi ya vikundi vitapatiwa wakufunzi wa kutengeneza maafuta ya Shampoo ambapo mpango huo utakuwa miezi mitatu.

Hata hivyo taasisi yake mbali ya kuwa na mpango huo pia itawapatia elimu ya namna ya kuziendesha shughuli zao kwa faida ili kuweza kuwa na marejesho na kuweza kuziendelea kazi zao   kukopa na kulipa kwa vikundi ambavyo vitatambulika.
 ‘Ndugu zangu akina mama, najua kuwa muko na uchu wa maendeleo ila nadhani munakwamishwa na pesa, sasa leo nawambieni kuwa Inuka inataka kuwaenua ninyi, jipangeni na kuwa na mshikamano ndani ya umoja wenu” alisema Msuya

Mkurugenzi wa Inuka imedhamiria kumuenu mjasiriamali ambaye anaonyesha dhamira ya kweli katika maendeleo ikiwemo kilimo na kazi nyengine za kimaendeleo ili kazi zake ziwe katika kiwango chenye ubora na kuweza kuuza bidhaa hizo ndani na nje katika masoko ya kimataifa.

Nia ya ujio wa ushirikiano wa soko la pamoja la Afrika Mashariki ni ukombozi mkubwa kwa wajasiriamali kuonyesha kazi zao na kuleta ushindani katika ubora wa bidhaa na kuweza kupata wateja na kuuza kwa faida.

Nae mmoja wa wajasiriamali hao, Hamida Vicent, ambaye ni mjasiriamali kutoka kikundi cha Tunasonga mbele amefurahishwa kuona kuwa kuna taasisi zinatambua uwepo wao mbali ya kuwa wako vijijini na hivyo kuitumilia fursa hiyo adimu waliopata.

“Awali walikuwa wakiendesha vikundi vyao na kutojua wapi wanaweza kupata mikopo na hivyo kikundi chao kikienda kwa kusuasua hivyo kwa sasa wamepata mwaga ambao utawawezesha kikundi chao kufika mbali.”