SIMULIZI ZA TABASAMU
PENDO LISILOISHA UTAMU.
Jamaa mmoja aitwae Mfalme alikuwa na mpenzi wake aliyempenda sana aitwae Malaika, walipendana sana hakuna mfano kila walipopita walionekana kweli wanapendana lakini katika maisha kuna kutafuta kwakuwa wawili hawa walikuwa bado hawajajitosheleza kimaisha hivyo kila mmoja alikwenda kuhangaika kwa upande wake.
Kwa upande wa Mfalme alikwenda kuongeza masomo yake huko nchi za nje alipata phd yake ya daktari kwa upande wa Malaika yeye alikwenda kupata master yake ya uhazili hapa hapa nchini, hivyo wawili hawa walipotezana kwa muda kadhaa bila mawasiliano yoyote lakini kila mmoja alikuwa na wazo la kumpata mwenzake endapo watakutana tena.
Mfalme alirejea nchini baada ya masomo yake hakuwa na haraka sana wa kufanya mawasiliano na Malaika kwakuwa alijua wapi angeweza kuampata mpenzi wake hivyo alichofanya aliyaandaa maisha yake kwanza kwa upande wa kusaka mali ili akimpata mwenza wake awe amejitosheleza kwa upande huo wa mali.
Alipoona kuwa sasa ni wakati wa kumsaka mwenza wake huyo alifika alipokuwa anaishi Malaika yaani nyumbani kwao, kwa bahati mbaya Malaika alishahama yeye na familia yake kwenda nchi nyingine kimaisha hivyo hakufanikiwa kumpata Malaika, lakini hakukata tamaa kwani alimpenda sana.
Siku moja hatika harakati za kumtafuta mwenza wake huyo alikumbuka kuwa walishawahi kupeana namba za simu hivyo alihangaika kutafuta ile namba ya simu kwenye makabdasha yake hapo nyuma na kufanikiwa kuipata namba ya Malaika wake, Mfalme alifurahi sana akawahabarisha familia yake nao walifurahi sana kwa kuwa walikuwa na hamu ya kuwaona wawili hao wakiwa pamoja kwenye maisha ya kifahari baada ya kuyatafuta.
Kwa upande wa wazazi wa Mfalme, walimshauri kijana wao kama asingeweza kumpata Malaika basi nibora aoe msichana mwengine kwani walikuwepo wasichana wengi tu wazuri ambao angeweza kuwaoa lakini kijana wao alikataa kabisa wazo na furaha yake ni kuishi na yule aliyempenda kwa dhati.
Siku na masaa yaliwadia Mfalme kuweza kuongea na mpenzi wake Malaika, wa ukeli aliyekaa kwenye moyo wake, akiwa kwenye jumba lake la kifahali lililojengwa pembeni kidogo na bahari lililokuwa limesheheni kwa kila kitu anachopaswa mtu kuishi, akiwa kwenye harakati hizo aliwaza jinsi ya kuanza kuongea naye kwa upande wa kukaa, yaani akae stari gani, awe ameweka maji pembeni, au awe amelala kitandani, ili tu aweze kuongea kwa pozi la aina yake, baada ya yote hayo alipata muafaka wa kuketi chini ya bustani yake yanye maua mazuri yenye yaliyotoa marashi ya kupendeza.
Jamaa akaanza kwa mbwembwe zote alizokuwa nazo, huku akiwa kwenye matengemeo ya kuweza kumpata Mlaika wake, mara akaisogeza kitabu chake chenye namba na kuaza kusoma namba moja moja kwa umakini, alipomaliza akaipiga namba ile bila kusita simu ikaita bila matengemeo yake, raha ilizidi kuongezeka na kimuhemuhe kikazidi kumjaa kijana, baada ya kusikia halololooo Mfalme wangu nimefurahi sana kweli unanipenda, sauti tu Malaika alijua kuwa ni Mfalme mpenzi wake.
Mfalme alishikwa na buttwaa kusikia kuwa mpenzi wake bado anaifahamu sauti yake ingawa ni kipindi kirefu mmno walichoachana na mpenzi wake huyo, aliishiwa nguvu lakini aliwa ameiengesha simu yake sikioni mwake hivyo alisikia maneno yote aliyokuwa anaongea Malaika wake, alidumu kwa muda wa masaa kadhaa bila kuongea kitu, mpaka aliporudi kwenye hali yake ya kawaida akaaza kuongea na mpenzi wake huyo.
MFALME: Kipindi kirefu sasa tangu tupotezane Malaika wangu upo wapi mpenzi wangu ninayekupenda kwa moyo wangu wote, niambiie mpenzi wangu kwa kuwa nilikutafuta sana baada ya kujiweka sawa kimaisha.
MALAIKA: Nipo kwenye ulimwengu mwingine rafiki yangu ulimwengu usiokuwa na mashaka, taabu, magonjwa, shida, na mengineyo, huko naishi kwa amani nikikusubiri mpenzi wangu kwa hamu uje tuwe pamoja milele.
MFALME: Niwapi huko mpenzi wangu kusikokuwa na matatizo yeyote ili niweze kuja tuwe pamoja kwenye maisha hayo uliyoyachangua, ila mpenzi wangu mimi huku nimeshajikamilisha kimaisha hivyo ukija huku tunaoana tu na tunaisha maisha ya raha milele, wewe unaonaje nije kukuchukuwa ili tuwe huku kimaisha, aliuliza.
MALAIKA: Huku nilipo kama nilivyokwisha kukuambia siwezi kuja tena huko kwani nipo kwenye ulimwengu mwingine mpenzi wangu kama wewe utakuwatayari niambie nije nikuchukue uje huku tuwe pamoja, lakini kabla sijaja kukuchukuwa inatakiwa uwahakarishe wazazi wako, ndugu, jamaa na marafiki na ukubari kuacha kila ulichotafuta huko kwakuwa huku utakuta vingi zaidi ya hivyo.
MFALME: Nipo tayari mpenzi wangu kuacha vyote nije tuwe pamoja, sitoweza kungangania mali na utajiri niliyonawo nikuache wewe mpenzi wangu, hivyo nipo tayari hata sasa njoooooo wangu kunichukua.
MALAIKA: Nitakuja usiku ukiwa umeshamaliza shughuli zako zote za kuaga na itakuwa muda mzuri kwa kuwa kesho yake itakuwa sherehe yako kubwa huko duniani.
MFALME: Sawa mpenzi wangu wa milelele yote
Mfalme alikubali bila kujua kuwa penzi wake huyo kwa maelezo aliyompa huko wapi, bila kutaka kujua baada ya masomo yake alifanya nini, yeye alijua kuitikia kwakuwa alikuwa anampenda sana, hakujua kuwa Malaika alifariki kitambo kirefu tu baada ya kumaliza masomo yake na umauti huo ulimpata baada ya kuondoka kwenda nchi nyingine na wazazi wake, kwa kuwa Mfalme alikuwa na shauku ya kuwa na mpenzi wake huyo, akutaka kujua mengi juu yake alitegemea wakiwa pamoja wataweza kuongea mengi.
Akiendelea kujiandaa mara wazazi wake walifika nyumbani kwake wakiwa na binti mrembo sana aliyefaria nguo yake ndefu ya heshima akiwa na furaha tele kumuona Mfalme.
Mfalme alishikwa na mshangao kuwaona wazazi wake kwa muda ule aliyowaambia kuwa anajiandaa kumlaki Malaika wake.
Wazazi wake walimtaka akae kidogo kwa maongezi, eeehe wazazi wangu huyu binti mrembo mmemtoa wapi na mbona mmemleta hapa nikiwa kwenye maandalizi yangu!
WAZAZI: Huyu ni binti wa pale jirani yetu anamaadili mazuri ya kupendeza ataweza kuishi na wewe kijana wetu tunayekutegemea sana.
MFALME: Mmmmm ni mzuri sana tena ni mrembo sana, lakini Malaika nimeshamkubalia kuja kunichukuwa hivyo sitaweza kuwa na pingamizi lolote juu yake wazazi wangu naomba mnisamehe sana, kwani nampenda sana na sitoweza kumuacha ikiwa nimemsikia kwa sikio langu mwenyewe bora nimfuate tukawe pamoja.
WAZAZI: Mbona hutusikiii sisi wazazi wako, kijana wetu tunayekupenda jua wewe ni kijana pekee wa kiume kwenye familia, usituache mwanetu, kwanza huyo Malaika hatujui kuwa yupo wapi ni kipindi kirefu sana hatujamuona kwenye maisha haya duniani, je kama atakuwa amefariki utaweza kumfuata huko aliko?
MFALME: Ndio wazazi wangu nitamfuata popote aliko kwani nampenda sana.
WAZAZI: Sisi hatuna la kufanya ngoja umsubiri huyo Malaika wako uende naye ingawa sisi wazazi wako umekubali unavyopenda wewe kijana wetu.
MFALME: Nashukuru sana wazazi wangu kwa kukubali jambo langu ninalilipenda la kuwa na Malaika wangu.
Wazazi wake waliondoka wakimuacha kijana wao wamsubiri Malaika wake wa milelele, wakiwa na huzuni na majozi kutokuwa na kijana.
Muda nao ulisogea Mfalme aliona kama Malaika wake anachelewa akitamani hata kumpigia tena simu ili amuulize amefikia wapi kuja kumchukua, lakini akajipa moyo kumsubiri, kwa sala na maombi yote asipatwe na mabaya wala pingamizi lolote anapokuja kumchukua.
Masaa yalifika Malaika alifika na kumtwaa aliyewake na kuondoka naye kwenye maisha ya milele yasiyokuwa na shida.
Upande wa wazazi wa Mfalme walilia sana kwa kuwa kijana wao hakupenda hata kuwasikiliza, hivyo walibaki na vilio na maombolezo makubwa sana.

MWISHO...........
Je ni wazazi wangapi wanaoweza kumtoa kijana wake apotee kwa sababu ya upendo na ikiwa wapo binti wengi ambao angeweza kuwaoa na kuishi nao kwenye maisha yote, lakini nao wameweza kuonyesha upendo wa dhati kwa kijana wao.
Kwa maisha ya sasa hapa duniani ni wangapi wanaoweza kumpenda mtu hadi kuamua kuacha mali zake na maisha yake ya kifahari kumfuata mwenzie bila kujali kufa na kupona ili mradi ampate anayempenda, wengi wa watu wamekuwa na upendo wa uongo na wengi wao wanampenda mtu eti tu ana mali nasinapoisha upendo huwa ni mwisho.
Upendo wa kweli haushawishiwi, haufundishwi, hauangalii, hauteteleki,huo ni upendo wa dhati kutoka moyoni, ukiona mtu anakupenda upendo kama huo bali ujue huyo ndie mwenzio, jirani,
rafiki na ndugu yako wa karibu sana.
TABIA MBAYA AAACHA:
Kuna watu wengine kwenye magari ya abiria huwa na tabia ya kumsogelea mwenzie hadi kumwachia edha inaweza kuwa marashi mazuri au mabaya, kutoka kwenye kwapa lake, yaani mimi nakerekwa sana na tabia hii, naomba wenye tabia hii waache mara moja sio nzuri.
Watu wengine si wastaarabu kabisa utakuta mtu anatembea mara kakohoa anatema lile kohozi lake bila hata kulifukia, au anapenga kamasi bila hata kufukia, huo si ustaarabu ni uchafu mtupu. Watu wenye tabia kama hii waache sio nzuri kwenye jamii.
WASIOCHEKA WAGUMU!
“Mtu mmoja anajifanya hapendi kucheka kabisa kwake mwiko, siku moja alipatikana na rafiki zake kwenye michemiche zao, kati ya wale rafiki zake mmoja akatoa stori ya kuchekesha wote wakacheka, sasa yule mgumu baada ya kucheka akatoa kojo kwa ajili ya kuzuia kucheka eeeeebwana mwenzie kutahamaki, wakaaza kumcheke yeye sasa, aangalia usije kuzuia kucheka na wewe ukatoa kinyesi badala ya kojo.”
Ushamba nao kazi,
“Mama mmoja aliyebahatika kuolewa na mzungu alingeuka kichekesho kwenye nchi za wenzetu baada ya kuchukua mtoto wake mtogo mwenye miezi kama mitatu hivi, kumuweka kwenye kitanda chake cha kuchezea akiwa kwenye kazi zake za nyumbani na kuanza safari yake ya kuelekea sokoni huku akiwa amekibeba kila kitanda kichwani kwa kuwa kimekaa kama kikapu. Haya sasa bora yeye ameweka kichwani mwezetu wengine wangebeba kile kama bidhaa na kutembea na mtoto bila hata wasiwasi.”
Msichana wa kazi za nyumbani nae,
“Mlezi wa mtoto aliyeaminiwa na bosi wake siku moja alitoa mpya ya mwaka baada ya kubembeleza mtoto mara bosi wake alipoelekea kazini, kambembeleza weweee mtoto hakunyamaza sasa akaamua ni bora nimuweke kwenye hili kabati ili akiona tu hawa kuku alioleta mama jana atanyamaza na mimi nitaendelea na kazi zangu, akamchukua yule mtoto wa miezi kadhaa ndani ya friji, mtoto alipohisi ile baridi arizidi kulia yeye hakujali akamfugia humu akaendelea na kazi zake, mara bosi akarudi akauliza mtoto yuko wapi, msichana nimemuweka kwenye hilo kabati la kuwekea kuku na nyanya ili anyamaze, hehehe haraka kwenda kuangalia mtoto siku nyingi kawa barafu. Inatakiwa kuwa makini na kupenda kutoa maelekezo kabla ya kuanza kazi.”
Hii nayo ni kali ya kustajabisha
“Jamaa mmoja aliamua tu kuondoka nyumbani kwake akiwa amejichora chora mwili mzima nia na madhumuni aweze kuchukuliwa na vyombo vya habari yaani auze sura, kweli waandishi walimpata kwa kuwa wao kazi yao ni kupata habari hivyo vyombo mbalimbali walimpiga picha na kumuuliza maswali kadhaa ya wakadhaa, hii nao mpya kama umaarufu unapatikana kwa njia hii bora mtu utulie tu kuliko kujidhalilisha namna hiii noma weeee”
“Haya sasa jamaa mmoja alijibadili yeye mwenyewe kujipiga picha baada ya kuzunguka huku na kule kukosa wateja wa kuwapiga picha hivyo kujigeuza yeye mwenyewe kuwa mpigaji na mpiga picha, akitembeatembea kwenye mitaa, mara akakutana na jambazi likampola kamera yake kwa kuwa alikuwa anaonekana kama chizi, yaangalie maisha yasije yakakupiga kama huyu jamaa baada ya kazi unaaza kuongea mwenyewe.”
“Jamaa mmoja aliamuakwenda kujibinafsisha kwa jirani akizani kuwa maisha yake yatakuwa ya ulahisi sana kumbe ilikuwa sivyo ndivyo, baada ya kuamua uwamuzi huo aliiambia familia yake wahamie kwa yule jirani yake, akifikili ataenda kuwa kama mfalme na familia yake, walipofika pale wakapewa masharti la kwanza kula chakula baada ya familia ile kushiba, kulala walwe wa mwisho baada ya familia ile kulala na masharti mengine mengi alipoona masharti yale ni magumu akaamua kuondoka kimnyakimnya bila hata kuoga.Watu wengine bwana wakiona maisha mazuri kwa wenzie wanayatamani badala ya kufanya kazi na kuboresha ya kwao, ukitaka cha mvunguni sharti uiname babake.”
...........KWA LEO TUSEME BASI..............
No comments:
Post a Comment