Saturday, December 31, 2011

MATUKIO MBALIMBALI

 Wafanyabiashara wa Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam, wakiuza ndizi kwa bei ya sh. 20,000 hadi 30,000 kwa mkungu.

 CHAGUA KICHANE KIMOJA SH. 2000 HADI 3000 MABIBO HAPA
 MATUNDA KAMA HAYO, VIWANDA VIKOWAPI TUOKOE MKULIMA WA MATUNDA KWA NYAKATI.
Mfanyabiashara wa kuuza vyungu vya kuwekea maua, Sospeter Jeremia, akitengeneza chungu katika eneo Kijitonyama Dar es Salaam jana, chungu kimoja ni kati ya sh. 30,000 hadi 40,000.
Wachezaji, Mack Gerald (7) na Darenn Kimari (5) wakifanya mazoezi  kwenye uwanja wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa Tenesi, Mussa Haruna,akiwafundisha wachezaji, Mack Gerald (7) na Darenn Kimari (5) wakifanya mazoezi  kwenye uwanja wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana

Saturday, December 17, 2011

MATUKIO MBALIMBALI

 Samaki wawili watu elfu itakuaje hapa.
Wafanyabiashara wa Soko la Feri jijini Dar es Salaam, wakisubiri kununua samaki kwa mnada katika soko hilo kwa bei ya sh. 30,000 hadi 35,000 kwa fungu.
Mfanyabiashara ndogondogo akisaka wateja katika sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam jana.

Saturday, December 10, 2011

MAANDAMANO YA MIAKA 63 YA HAKI ZA BINADAMU


Ndio tunajiandaa, maandamano ya maadhimisho ya miaka 63 ya haki za binadamu duniani yaliyofanyika Dar es Salaam jana.





Bendi ya Jeshi la Magereza wakiburudisha wakati wa maandamano ya maadhimisho ya miaka 63 ya haki za binadamu duniani yaliyofanyika Dar es Salaam jana.  


Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, akiwa ameshika bango lenye ujumbe, wakati wa maandamano ya maadhimisho ya miaka 63 ya haki za binadamu duniani yaliyofanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen Kijo Basimba.

KUWEKA AKIBA NA KUKOPA TANDALE SACCOS

Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo wa soko la Tandale (TANDALE SACCOS), wakiwa kwenye mkutano mkuu wa chama chao uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.


Saturday, November 26, 2011

YANAYOTOKEA

Kikundi cha Ngoma cha JKT Mgulani wakiburudisha kwenye maonyesho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Ofisi ya Rais katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa tenesi, Grace Laymond, (13) akipiga mpira wakati wa mashindano ya BQ Open yaliyoanza kwenye viwanja vya Gymkhana Club Mjini Dar es Salaam jana.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakifuatia kwa makini kongamano la hali ya elimu Nchini miaka 50 baada ya uhuru lililofanyika kwenye Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana.