Saturday, April 30, 2011

CHEKA KIDOGO LEO.

Leo si siku ya wenye mabavu hapana bana nimekoseaa tu ng’oja nikupe stori ya ukweee, jamaa moja lilikuwa linasikia, sijui linahisi njaa silikaamua kwenda kwa mama nijazie lilipofika kule likala hadi likavimbiwa likaaza kuumwa tumbo badala ya kudaiwa pesa likapelekwa hospitalini kwa matibabu ya tumbo, jamaa balaaa weeee!

PATA BURUDANI NA EXTRA BONGO

 WANAUME wapo kazini.
 Wadada nao hawajarudi nyuma burudani kwa kwenda mbele.



 Hadi vuvuzela nalo lipo ndani ya extra bongo.
 Mambo hayo...........
sasa UNAKARIBISHWA na wewe kuburudika na extra bongo.

JINSI MAONYESHO YALIVYOFUNGWA

 Wanachuo wakipata maelekezo kutoka kwa mwalimu


 Wanafunzi nao hawakurudi nyuma




Maelezo yanaendelea

MKUTANO WA MASHIRIKA YASIYOYAKISERIKALI

 Umejiona baba ulivyotulia kama upo kwenye maswali.
 Washiriki wengine kwenye mkutano huo uliyoitishwa na Benki ya Dunia.


Wapo bize kwenye mkutano.

Thursday, April 28, 2011

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, (Kulia)akifafanulia jambo na Afisa Uhusiano wa Chuo Kikuu cha St. John’s, Karimu Meshark,  wakati wa kutembelea katika banda lao la  maonyesho ya sita ya Vyuo Vikuu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

KUTOKA ZANZIBAR

Maonyesho yamepamba moto.

MAONYESHO YA SITA YA VYUO VIKUU



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akikabidhiwa zawadi wakati wa maonyesho ya sita ya Vyuo Vikuu yanayoendelea kufanyika katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Saturday, April 23, 2011

Baadhi ya wakazi wa eneo la Tandale kwa Tumbo, jijini Dar es Salaam., wakitafakari jinsi ya kukatisha katika barabara iliyojaa maji ya mvua yaliyochanganyikana na kinyesi jana.
Mwendesha pikipiki (bodaboda) akijaribu kumpitisha mteja wake bila kujali maisha yao kwenye maji yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu nyingi jijini Dar es Salaam. 

MVUA HIYO.

Gari lenye namba za usajili T 273 APA, likiwa limezama kwenye mtaro uliotuama  maji ya mvua, eneo la Samaki jijini Dar es Salaam jana. Mitaro mingi haifanyiwi usafi na manispaa za jiji la Dar es Salaam, ambapo husababisha maji kutuama hata kama mvua ni kidogo.

MAMBO YA SIKUKUU HAYO.

Wafanyabiashara wa mbuzi  eneo la vingunguti jijini Dar es Salaam, wakiwasubili wateja  wa kununua mbuzi ambao walikuwa wakiuzwa kuanzia Sh  90,000 na 120,000 kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka . Picha na Deus Mhagale.

Friday, April 22, 2011