Saturday, July 30, 2011

WANAWAKE TUAMKE KWA PAMOJA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya My Solidarity Investment, Lucy Mchonko, akizungumza na wajasiriamali Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano  wa wajasiriamali kutoka taasisi mbalimbali  ulioandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Twende.

Akina mama wakiwa wamejitwisha mikungu ya ndizi katika eneo  la Kiwila mkoani Mbeya, kwa ajili ya kuwauuzia wateja wanaopita katika eneo hilo. Mkungu mmoja wa ndizi unauzwa kati ya Sh 3,000 hadi Sh 4,000.

             

Friday, July 29, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE YALIVYOKUWA KIGAMBONI DAR ES SALAAM JANA.

 Hapa ni VIONGOZI wa siasa kutoka vyama vya siasa mbalimbali Nchini.
 Juu ni Wanafunzi waliopitia katika CHUO hicho enzi za MWALIMU
 Aliyekuwa mkuu wa CHUO hicho akitoa naye maoni yake kwenye mdahalo
 Mwakilishi kutoka Chama cha TLP, GETRUDA PWILLA akitoa maoni yake kwenye mdahalo
Wanafunzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere, wakishangili baadhi ya hoja zilizokuwa zikitolewa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho na kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, yalifanyika chuoni hapo Kigamboni Dar es Salaam.
 Naye mwakilishi kutoka CHAMA CHA NCCR - MAGEUZI, JUJU MARTIN DANDA akitoa maoni kwenye mdahalo.
 PICHA ZA PAMOJA NDIO HIZO


 MAONYESHO YA MACHAPISHO MBALIMBALI YANAYOONYESHA VIONGOZI MBALIMBALI





 PICHA YA PAMOJA NA BENDI YA ENZI HIZO SIKINDE.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mwalimu Nyerere, Dk. Salim Ahmed Salim (kulia) akitoka kwenye ukumbi wa sherere baada ya kufikia mwisho wa maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho pamoja na kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, yaliyofanyika chuoni hapo Kigamboni Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Dk. John Magotti.
 Bendi kutoka JESHI LA POLISI NAO WALIKUWEPO kuburudisha.
Wanamuziki wa bendi ya Sikinde, Yusuph Bernad(kulia) na Shabani Lendi (kushoto) wakitumbuiza siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jana. 
HASSANI KUNYATA miongoni mwa wanamuziki wa bendi ya Sikinde akiimba siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja na kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jana. 

Thursday, July 28, 2011

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA PAMOJA NA WAZEE KILICHOPO CHINI YA KANISA KATOLIKI MSIMBAZI DAR ES SALAAM.

 HAPA NI KIWANGO CHA TANO
 KIWANGO CHA PILI
 KIWANGO CHA KWANZA
 KIWANGO CHA MWISHO

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Good Samaritan ya Dar es Salaam, Aurelia Nkungu (kulia), akiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza waliotoa msaada.



Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Good Samaritan ya Dar es Salaam, Aurelia Nkungu (kushoto), akimkabidhi Sister Cyirila Kessy, ambaye ni msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre cha Dar es Salaam, katoni za sabuni na bidhaa mbalimbali zilizotolewa na  wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo jana.


Na. Otilia Paulinus
WANAFUNZI wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Good Samaritan iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam jana walitoa misaada yenye thamani ya sh. 700,000 kwa watoto yatima na wazee wasiojiweza wanaolelewa na Kituo cha Msimbazi.
Kituo hicho, ambacho kipo chini ya Kanisa la Katoliki, kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu wa fedha za kujikimu pamoja na chakula kwa watoto wadogo na wazee.
 Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Sista Mkuu Cyirila Kesi, ambaye pia ni Mama Mlezi wa kituo hicho alisema kuna ukosefu mkubwa wa fedha za kujikimu kwani kituo hicho hutegemea msaada kutoka kwa wasamaria wema.
“Kituo chetu kinalea watoto 44 na wazee 40 wasiojiweza ambao hawana msaada kutoka sehemu mbalimbali nchini na hutegemea misaada kutoka kwa wasamaria wema ili kusaidia kuwalipa  wafanyakazi na matibabu kwa wazee pamoja na watoto ,”alisema Sista Kesi.
Naye mwakilishi wa wanafunzi hao, Sabra Nazir alisema msaada huo ni sehemu ya mchango wao kwa wototo na wazee wanaolelewa kituoni hapo na aliiomba jamii kuwa na moyo wa kutoa kwa wale wanaohitaji msaada.
 Msaada tulioutoa ni mdogo hivyo tunaziomba taasisi binafsi na mashirika mbalimbali wawe na moyo wa kuwajali wazee kwa kuwapa misaada kwa kuwa wazee wengi wametelekezwa na ndugu zao,”alisema Nazir.

Msaada walioutoa ni pamoja na mashuka, sabuni, unga, nguo, viatu, na vitu vingine.

Saturday, July 23, 2011

Buriani Dany Mwakiteleko


Marehemu Danny  enzi za uhai wake


Marehemu Danny akiwa hospital
MHARIRI wa gazeti la Rai, ambaye pia ni Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari, Danny Mwakiteleko, amefariki dunia. Habari ambazo blogu hii imezipata leo alfajiri na kuthibitishwa na watu wa karibu zinasema kwamba Mwakiteleko amefariki leo alfajiri katika hoispitali ya Muhimbili. Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahtuti Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku (jumatano) eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.

Thursday, July 21, 2011

JAMII YETU

 Wanawake wajasiliamali kutoka kijiji cha Bihawana mkoa wa Dodoma, wakiwa na bidhaa zao baada ya kushuka kwenye daladala wakisaka wateja wa kununua bidhaa, hapa wakipita barabara ya stendi  Dodoma hivi karibuni.

SIKU YA WIKI YA MAONYESHO YA MALIASILI NA UTALII YALIVYOKUWA KATIKA MAKUMBUSHO YA TAIFA DAR ES SALAAM

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, MaimunaTarishi
Akisalimiana na wafanyakazi wa makumbusho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, akisaini kwenye daftari la wageni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi, akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Jackson Kihiyo. Wakati wa kilele cha maonyesho ya maliasili na utalii yaliyofanyika Dar es Salaam jana.