Saturday, July 2, 2011

NB:MATUKIO MBALIMBALI PAMOJA NA JAMII YETU

 Msimamizi wa nyumba za wageni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Nashi Mnzava. (katikati) na Mkuu wa Shule hiyo, Major. Celestine Mwangasi, Mfadhili wao, Federick Freeman (nyuma) pamoja na viongozi wengine wa Shule ya Sekondari Makongo na Shule ya Msingi Changanyikeni wakitembelea sehemu za Shule hiyo.
Wanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Makongo wakimsikiliza Mfadhili wao, Frederick Freeman,kutoka Marekani ambaye hayupo pichani akiwaeleza jambo alipotembelea darasa hilo ambalo ni moja wapo lilipata msaada wa computer kwa ajili ya kujifunzia wakati wa hafla iliyofanyika Shuleni hapo jijini  Dar es Salaam jana. 
 Wimbo wa Taifa kwa ajili ya kumkaribisha mgeni.
 ZAWADI ANAPEWA NA UONGOZI WA SHULE
Mfadhili kutoka Marekani, Federick Freeman, akiwa ameshika zawadi ya Kinyango chenye muundo wa Ramani ya Afrika aliyokabidhiwa na Uongozi wa Shule ya Sekondari Makongo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa Computer, Meza ya kucholea na Viti kwa wanafunzi wa shule ya Awali ya Changanyikeni iliyofanyika shuleni hapo jana. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Major. Celestine Mwangasi. Kulia ni Msimamizi wa nyumba za wageni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Nashi Mnzava.  
Federick Freeman akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
 Msaada sasa wanakabidhiwa kama hivi.
 MNAONA
 PICHA YA PAMOJA NA Wanafunzi wa Shule ya Msingi Changanyikeni
 PICHA YA PAMOJA WA UONGOZI WA SHULE ZOTE MBILI


 MAMBO YA BURUDANI KAMA HIVI
Kikundi cha burudani kutoka Shule ya Sekondari Makongo, Dar es Salaam, kikitumbuiza kwenye hafla ya makabidhiano ya vifaa vya msaada kwa shule hiyo na Shule ya Msingi Changanyikeni, yaliyofanyika Dar es Salaam jana. Vifaa hivyo vilitolewa na Mfadhili, Frederick Freeman, kutoka Marekani. 
MAMBO YA UVUVI KATIKA SOKO LA FERI DAR ES SALAAM.



 Wanauzwa sasa kwa bei ya sh. 1000 kwa fungu ama kindoo
 MAMBO YA BIASHARA KATIKA SOKO LA MABIBO DAR ES SALAAM
 Mfanyabiashara katika soko la Mabibo jijini Dar es Salaam, akiweka sawa biashara yake tayari kwa kuwauzia wateja wake kwa siku hiyo, ikiwa kila ndoo ya viazi ni kati ya sh. 10,000 hadi 9,000
 Bei ya ndizi kwa sasa ni kati ya sh. 5,000 hadi 3, 000 kwa mkungu ni sh. 25,000 hadi 20,000
 Mfanyabiashara mwanamama akiwa kwenye kuweka sawa biashara ya machungwa ambayo yanauzwa kati ya sh. 70 hadi 50 kwa bei ya jumla katika soko la Mabibo Dar es Salaam.
Tikiti ni tunda bora sana wa wagonjwa na watu wazima kwa sababu maji yake ni tosha kabisa kwa afya ya mtumiaji yanapatikana katika soko la Mabibo kwa bei ya Sh. 2000 na 1000 jumla, mnakaribishwa kwa afya bora.

No comments:

Post a Comment