Thursday, July 28, 2011

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA PAMOJA NA WAZEE KILICHOPO CHINI YA KANISA KATOLIKI MSIMBAZI DAR ES SALAAM.

 HAPA NI KIWANGO CHA TANO
 KIWANGO CHA PILI
 KIWANGO CHA KWANZA
 KIWANGO CHA MWISHO

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Good Samaritan ya Dar es Salaam, Aurelia Nkungu (kulia), akiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza waliotoa msaada.



Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Good Samaritan ya Dar es Salaam, Aurelia Nkungu (kushoto), akimkabidhi Sister Cyirila Kessy, ambaye ni msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Msimbazi Centre cha Dar es Salaam, katoni za sabuni na bidhaa mbalimbali zilizotolewa na  wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule hiyo. Makabidhiano hayo yalifanyika kituoni hapo jana.


Na. Otilia Paulinus
WANAFUNZI wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Good Samaritan iliyoko Masaki jijini Dar es Salaam jana walitoa misaada yenye thamani ya sh. 700,000 kwa watoto yatima na wazee wasiojiweza wanaolelewa na Kituo cha Msimbazi.
Kituo hicho, ambacho kipo chini ya Kanisa la Katoliki, kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu wa fedha za kujikimu pamoja na chakula kwa watoto wadogo na wazee.
 Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Sista Mkuu Cyirila Kesi, ambaye pia ni Mama Mlezi wa kituo hicho alisema kuna ukosefu mkubwa wa fedha za kujikimu kwani kituo hicho hutegemea msaada kutoka kwa wasamaria wema.
“Kituo chetu kinalea watoto 44 na wazee 40 wasiojiweza ambao hawana msaada kutoka sehemu mbalimbali nchini na hutegemea misaada kutoka kwa wasamaria wema ili kusaidia kuwalipa  wafanyakazi na matibabu kwa wazee pamoja na watoto ,”alisema Sista Kesi.
Naye mwakilishi wa wanafunzi hao, Sabra Nazir alisema msaada huo ni sehemu ya mchango wao kwa wototo na wazee wanaolelewa kituoni hapo na aliiomba jamii kuwa na moyo wa kutoa kwa wale wanaohitaji msaada.
 Msaada tulioutoa ni mdogo hivyo tunaziomba taasisi binafsi na mashirika mbalimbali wawe na moyo wa kuwajali wazee kwa kuwapa misaada kwa kuwa wazee wengi wametelekezwa na ndugu zao,”alisema Nazir.

Msaada walioutoa ni pamoja na mashuka, sabuni, unga, nguo, viatu, na vitu vingine.

No comments:

Post a Comment