Saturday, July 2, 2011

SABASABA HIYO..

Wananchi mbali mbali wakiwaangalia Kobe wakubwa katika Bustani ya Wanyama, kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Ufundi wa Mashine ya Kuvuna Mpunga (KUBOTA Harvester Mashine), Hussein Sadi, akimuelekeza mmoja wa wananchi waliofika katika Banda la Zana za Kilimo (Farm Equipment) jana mchana kwenye maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Mashine ya KUBOTA Harvester inavuna na kupeta mpunga kwa kiasi cha hekali kumi kwa siku.
Afisa Uhamiaji, Sophia Gunda, akimfafanulia jambo jana mwananchi aliyefika Banda la Idara ya Uhamiaji katika Maonesho ya 35 ya Kimataifa ya Biashara,  sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Picha zote na Victor Makinda
MAMBO YA KATIBA MPYA.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, akizungumza na waandishi wa habari  mjini Dar es Salaam jana, kuhusu mafikio ya mchakato wa kuweka utaratibu wa kupata katiba mpya ambayo itashirikisha jamii nzima. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya.

No comments:

Post a Comment